1 Desemba 2025 - 22:37
Jibu la Ayatollah Al-Udhma Sistani Kuhusu Kufuata Maimam wa Sala ya Jamaa  Wanaopokea Malipo (Mishahara) za Kiserikali

Ayatollah Al-udhma Al-Sistani, kiongozi mkuu wa Shi’a, katika jibu lake kwa swali kuhusu kufuata maimamu wa sala ya jamaa (imam wa jamaa) wanaopokea haki (ya mishahara) kutoka serikali za Kiislamu, alishauri waumini wasisali nyuma yao, ili nafasi za kidini zilindwe dhidi ya uingiliaji wowote unaowezekana wa serikali.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Swali limeulizwa kwa Ayatollah Al-Udhma Al-Sistani: "Katika baadhi ya nchi za Kiislamu, serikali hutoa mshahara wa kila mwezi kwa maimamu wa sala katika misikiti, na baadhi yao ni wanadini wa Shi’a. Maoni yako ya heshima kuhusu hili ni yapi?"

Katika jibu lake, alisema:
"Tunashauri waumini (Azzahum Allah Ta’ala) wasisali nyuma ya mtu anayepokea mshahara wa kiserikali. Hili si kwa sababu ya kumdhalilisha au kumshutumu juu ya haki zake, bali ni ili nafasi hizi na hadhi za wamiliki wake zikubalike kuwa salama dhidi ya kuingilia kati kwa serikali yoyote inayoweza kutokea, hata siku zijazo."

Matini ya swali na jibu kwa Kiarabu ni kama ifuatavyo:

السؤال: فی بعض الدول الإسلامیة تخصص الحکومة راتباً شهریاً لأئمة الجماعة فی المساجد وقسم منهم من رجال الدین الشیعة، فما هو نظرکم الشریف بهذا الخصوص؟

الجواب: ننصح المؤمنین (أعزّهم الله تعالی) أن لا یصلوا خلف من یتقاضی راتباً حکومیاً، ولیس هذا للقدح فیه والطعن فی عدالته، ولکن لتبقی هذه المواقع ومواقف أصحابها بمنأی تام عن أی تدخل حکومی محتمل ولو فی مستقبل الأیام.

Swali: Katika baadhi ya nchi za Kiislamu, serikali hutoa mshahara wa kila mwezi kwa maimamu wa sala katika misikiti, na baadhi yao ni wanadini wa Madhehebu ya Shi’a. Maoni yako ya heshima kuhusu hili ni yapi?.

Jibu: "Tunashauri waumini (Azzahum Allah Ta’ala) wasisali nyuma ya mtu anayepokea mshahara wa kiserikali. Hii si kwa sababu ya kumdhalilisha au kumshutumu juu ya uadilifu wake, bali ni ili nafasi hizi na hadhi za wamiliki wake zikubalike na kuwa salama dhidi ya kuingiliwa na serikali yoyote iile nayoweza kutokea, hata katika siku zijazo".

Uhakikisho wa uhuru wa nafasi za kidini

Jibu hili linaonyesha msisitizo wa kiongozi wa juu wa Shi’a juu ya umuhimu wa uhuru wa nafasi za kidini na kulinda nafasi hizo dhidi ya kuingilia kati au ushawishi wowote unaowezekana wa serikali.

Chanzo Rasmi:
Hili swali na jibu limechapishwa kwenye tovuti rasmi ya Ayatullah Kiyama Al-Sistani:
https://www.sistani.org/arabic/qa/02756/#26952

Jibu la Ayatollah Al-Udhma Sistani Kuhusu Kufuata Maimam wa Sala ya Jamaa  Wanaopokea Malipo (Mishahara) za Kiserikali

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha